Mtoto Akaunti

Hii ni akaunti ya Wajibu inayokuwezesha kumuwekea mtoto wako akiba kuanzia miaka 0 mpaka 12. Ni akaunti itakayomjengea msingi imara kwenye malezi na elimu yake ya kifedha. Utafurahia manufaa yafuatayo kwenye akaunti hii:

 • Hakuna gharama za kuendesha akaunti
 • Unaweza kuweka akiba muda wowote na mahali popote Tanzania kupitia NMB Wakala, NMB Mobile au kwenye matawi yetu
 • Unaweza kupata pesa wakati wowote, popote
 • Viwango vya riba vyenye mvuto

Unahitaji vitu vichache kufungua akaunti yako:

 • Kitambulisho cha mzazi au mlezi kinachotambuliwa kisheria
 • Barua ya utambulisho wa mzazi au mlezi kutoka serikali ya mtaa au mwajiri
 • Hati ya kusafiria, kiapo cha mahakama au cheti cha kuzaliwa cha mtoto
 • Picha mbili  za pasipoti zenye background ya bluu za mtoto zilizopigwa karibuni
 • Salio la kufungulia la TZS 5000

 

Chipukizi Akaunti

Akaunti ya Chipukizi ni maalum kwa watoto kuanzia miaka 13 mpaka 17. Inawasaidia kuratibu pesa zao chini ya uangalizi wako, huku ikiwajengea uwezo wa kutumia pesa kwenye maisha yao ya baadae. Utafurahia faida zifuatazo ukiwa na akaunti hii:

Manufaa:

 • Standing order za bure
 • Gharama nafuu za kuendeshea akaunti
 • Inapatikana kwa sarafu za nyumbani na za kimataifa
 • Viwango vya riba vyenye mvuto

Unahitaji vitu vichache tu kufungua:

 • Kitambulisho cha mzazi au mlezi kinachotambuliwa kisheria
 • Barua ya utambulisho wa mzazi au mlezi kutoka serikali ya mtaa au mwajiri
 • Hati ya kusafiria, kiapo cha mahakama au cheti cha kuzaliwa cha mtoto
 • Picha mbili za pasipoti zenye background ya bluu za mzazi au mlezi zilizopigwa karibuni
 • Salio la kufungulia la TZS 2000

 

Mwanachuo Akaunti

Wakati kijana wako akiendelea kipiga hatua kimasomo kuelekea kwenye ndoto na malengo yake, Mwanachuo akaunti inamsaidia kuweka akiba na kupanga matumizi kwa uhuru. Huu ni muda wake wa kutengeneza uwiano mzuri kati ya maisha na masomo.

Utahitaji yafuatayo ili kufungua akaunti yako:

 • Kitambulisho cha chuo kinachotumika
 • Barua ya utambulisho kutoka chuoni
 • Picha mbili za pasipoti zenye background ya bluu na zilizopigwa hivi karibuni
 • Salio la kufungulia akaunti la TZS 10,000