KUHUSU NMB WAJIBU?

NMB inaamini kwamba ni jambo la busara kupanga mikakati ya kifedha kuanzia utotoni, na hii ndiyo sababu ya kushirikiana na Women’s World Banking kukuletea akaunti ya Wajibu – akaunti maalum ya kuweka akiba kwa vijana na watoto kwa ajili ya maendeleo ya baadae.

MAALUM KWA AJILI YAKO

Maalum kwa ajili yako

Mwanachuo Akaunti

Wakati kijana wako akiendelea kipiga hatua kimasomo kuelekea kwenye ndoto na malengo yake, Mwanachuo akaunti inamsaidia kuweka akiba na kupanga matumizi kwa uhuru. Huu ni muda wake wa kutengeneza uwiano mzuri kati ya maisha na masomo.

Utahitaji yafuatayo ili kufungua akaunti yako:

  • Kitambulisho cha chuo kinachotumika
  • Barua ya utambulisho kutoka chuoni
  • Picha mbili za pasipoti zenye background ya bluu na zilizopigwa hivi karibuni
  • Salio la kufungulia akaunti la TZS 10,000